TAHADHARI YA MKOJO



 TAHADHARI KUHUSU MKOJO

Assalaam alaykum.
Naomba tukumbushane kuhusiana na najisi ya mkojo.Mkojo ni moja ya najisi ambayo baadhi yetu huichukulia ni ya kawaida sana.Haishangazi kuona mtu atakapo kuswali huenda haja ndogo mara baada ya sekunde chache kutoka msalani na kuchukua udhu kwa ajili ya swala!.
TAHADHARI.
Mfano wa mkojo ni kama maji yaliyo kwenye sahani ya dongo au bati.Pindi ukiyamwaga maji hayo kamwe sahani haitokuwa kavu kwa muda huo na baada ya muda kidogo utaona maji yamebaki.
Hivyo hata unapoenda kujisaidia haja ndogo unatakiwa uchukue mfano huo ili nguo yako usije najisika na kuharibu swala yako.Baada ya kujisaidia chukua muda kidogo na usifanye haraka hata km unataka kuwahi swala.
Kumbuka ukamilifu wa swala upo kwenye twahara.

Comments

Popular posts from this blog

NIA YA KUOGA ILI KUONDOA JANABA,HEDHI NA NIFASI

MAMBO YALIYOHARAMU KWA MWENYE JANABA,HEDHI NA NIFASI