ZAKATUL FITIR:MAANA YAKE,ANAEWAJIBIKA KUTOA NA NAMNA YA KUITOA
Tupo kwenye kumi la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,mbali ya usiku bora kabisa wa Laylatul Qadir kupatikana kwenye kumi hili la mwisho lakini pia ndio kumi ambalo Waumini huwa wanakumbushwa watoe Zakatul Fitir ZAKATUL FITIR NI NINI? Zaka ya Fitir ni Ibada kwa Muislam kutoa kiasi cha chakula kumpa masiki kuelekea mwisho wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani,na mwisho wa kutoa Zakatul Fitir ni kabla ya kuswaliwa swala ya Iddi.Iwapo mtu atatoa baada ya swala ya Eid hiyo haitokuwa Zakatul Fitir bali Itakuwa Swadaqa kama swadaqa zingine. NANI ANAEWAJIBIKA KUTOA ZAKATUL FITIR? Kila Muislam Baleghe na mwenye akili timamu ambae kuelekea kwenye sikukuu bajeti yake ya chakula imetosheleza na imezidi hivyo kile kilichozidi anatakiwa akitoe kama Zakatul Fitir kwa kumpa Masikini. Kiongozi wa Familia atajitolea yeye na wale waliochini yake(anaowamiliki)kama Mke,watoto,mfanya kazi na wengine lakini pia anaweza kuwatolea wazazi au ndugu wengine km akiwa na uwezo wa kufanya hivyo.Katika watoto...