IJUE TWAHARA
Twahara ni kitendo ambacho pindi kitakapokosekana haitoswihi swala.
Twahara imegawanyika sehemu kuu 2.
1.Twahara kubwa
2.Twahara ndogo
1.TWAHARA KUBWA.
Hii inahusisha ukogaji kwa taratibu maalimu ikiwemo nia ya kuoga ili kuondoa hali husika na kutwaharika.
Hali zinazomlazimu mtu kuoga ili kutwaharika ni 4
>Janaba
>Hedhi
>Nifasi
>Mauti
JANABA
Janaba ni hali ambayo humkuta mwanamme au mwanamke.
Sababu zinazopelekea mtu kuwa na janaba ni-:
>Kutokwa na manii{shahawa}iwe kwa makusudi au bahati mbaya kama vile kuota,mfadhaiko.kukutana kimwili,kujichua{punyeto au kujisaga}
>Kuingilia au kuingiliwa kimwili,pindi mtu atakapoingilia au kuingiliwa kimwili itakuwa amepata Janaba,Haijalishi kama atakuwa ameingilia au kuingiliwa kwa makubaliano au kulazimishwa{kubaka au kubakwa}awe amemuingilia au kuingiliwa na binaadamu au kiumbe mwingine km Jini au mnyama.
>Kukutanisha tupu mbili,endapo mtu ataugusisha tupu yake kwenye tupu nyingine atakuwa amepata janaba hata km hatotoa manii{shahawa}haijalishi km tupu imeingia au imegusa nje tu.Mtu akikutana na hali hiyo atakiwa akoge kwa nia husika na taratibu maalumu na josho hilo huitwa JANABA.
HEDHI
>Hii humkuta mwanamke pale anapokuwa ameingia kwenye damu ya mwezi{hedhi/period}Pale damu inapoanza kutoka mwanamke huyo anahesabika ana hedhi na ili atwaharike atalazimika akoge kwa nia na utaratibu maalumu ili kuuweka mwili wake safi pale atakapomaliza siku zake.Haijalishi km damu ilitoka kawaida,ilizidi au ilitoka kidogo atalazimika kukoga na josho hili huitwa HEDHI.
NIFASI
>Nifasi humkuta mwanamke ambae amejifungua,mwanamke anapojifungua hutokwa na damu na damu hiyo huitwa damu ya Nifasi na mwanamke huyo baada kukata atatakiwa kuoga kwa nia na utaratibu maalumu ili kuweka mwili wake safi na josho hilo huitwa NIFASI.

Comments
Post a Comment