NAMNA YA KUOGA KWA NIA MAALUM ILI KUTWAHARIKA.NO:1
Kuna njia mbili za kuoga nazo ni:-
>Faradhi peke yake{Njia fupi}
>Faradhi na sunna{Njia ndefu}
Kwenye sehemu hii ya kwanza tutajifunza Faradhi za kuoga
Faradhi za kuoga zipo 2
>Nia ya josho husika
>Kueneza maji mwili mzima
Aogae anatakiwa anuie josho analotaka kuoga km Janaba,Hedhi au Nifasi.Nia ya muogaji iende sambamba na kuanza kujimwagia maji na ahakikishe mwili wake wote unapata maji.
MAANDALIZI YA KUKOGA.
Tumeshatambua kuwa muogaji atanuia huku akijimwagia maji na ahakikishe mwili wote unaenea maji sasa tuangalie maandalizi ya maji na mwili kwa ujumla.
Andaa ndoo safi kwa ajili ya kuogea kisha weka maji safi na hakikisha hauyatii mkono wala kidole.
Andaa kata ya kuogea au kitu jingine ambacho pindi utakapokuwa unakoga maji hayatoweza kuchuruzika na kurudi kwenye ndoo ya maji.
Hakikisha mwili wote hauna kitu ambacho kitazuia maji kufika kwenye ngozi km vile wigi,nywele nyingi zilizosukwa,rangi kwenye ngozi au kucha,Rami nk.
Baada ya maandalizi hayo utajisaidia haja ndogo ili kuondoa mabaki ya Manii{Shahawa au Damu}.Kisha fuata utaratibu huu:-
>Nuia nia husika huku ukijimwagia maji kuanzia kichwani
>kisha jimwagie upande wa kulia mara 3 huku ukinuia
>kisha upande wa kushoto mara 3 huku ukinuia
NB:Hakikisha sehemu zote zipate maji na na kila upotaka kutia maji unuie kwani nia na kitendo vinatakiwa vifuatane hivyo kunuia na kijimwagia maji viambatane.
NIA YA KUKOGA JANABA
>Nawytu rafa'aal janaba{Nanuia kuondoa Janaba}
NIA YA HEDHI
Nawaytu twaharata minal haidhwi{Nanuia kutwaharika na hedhi}
NIA YA NIFASI
Nawaytu twaharata mina nifasi{Nanuia kutwaharika na nifasi}
Kumbuka hapo awali tulisema josho la mwanamme ni janaba tu laki mwanamke anaweza akawa na majosho yote.Iwapo itatokea mwanamke ana Hedhi na Janaba au ana Hedhi,Janaba na nNifasi au mawili kati ya majosho hayo basi anaweza akatumia nia moja na akatwaharikana majosho yote matatu kwania moja na kwa kukoga mara moja.
Ila atanuia nia hii"Nawaytu adaa furdhwul ghusilu"{Nanuiya kutekeleza faradhiya kuoga}
Mahali pa nia ni moyoni na nia huambatana na kitendo lakini pia hakikisha mwili wote unaenea maji kwa kuanzia kichwani,upande wa kulia na kumalizia upande wote wa kushoto.Hakikisha mwili wako unaugawa kwenye hizo sehemu 3,pia tahadhari maji yanayoanguka chini au kuchuruzika yasiingie kwenye maji yaliyo kwenye ndoo.
Ubora wa nia kuihifadhi na kuitamka moyoni.
Km maji yatatoka moja kwa moja bombani itakuwa bora zaidi naa utafuata utaratibu uleule na wala haina haja ya kutumia ndoo au kata ya maji
.jpg)
Comments
Post a Comment