UJUE USIKU WA LAYLATUL QADIR
LAYLATUL QADIR ni Usiku bora kabisa ambao hupatikana kwenye kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani.Ubora wa usiku huu ALLAH Subhanahu wataalaa ameutaja kwenye Qur'an kwa kusema"
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾
Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatil-Qadr (usiku wa Qadar).
وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾
Na nini kitakachokujulisha ni nini huo Laylatul-Qadr?
لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾
Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.
تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾
Wanateremka humo Malaika na Ar-Ruwh (Jibriyl) kwa idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.
سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾
Amani mpaka kuchomoza Alfajiri. [Al-Qadr: 1-5]
Muislam anatakiwa afanye bidii kwenye kumi ili la mwisho kwa kufanya ibada za usiku ili kuweza kuupata usiku huo.Kwani mwenye kuipata Laylatul Qadir atalipwa thawabu za miezi alfu moja{1000}Miezi elfu moja ni sawa na miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban. (1000 ÷ 12 = 83.3)
Utakapokuwa umo katika ‘ibaadah usiku huo wa Laylatul-Qadr, basi utaandikiwa thawabu za miaka 83! Juu ya hivyo, ‘ibaadah ya usiku huo ni bora zaidi kuliko ‘ibaadah ya miaka themanini na tatu.
Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu fadhila za usiku huu mtukufu na jinsi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan
Mwenye kuikosa Laylatul Qadir atakuwa amepata hasara kubwa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ilipofika Ramadhwaan, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Umekujieni mwezi wa Ramadhwaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni fardhi, milango ya Jannah hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa. Katika mwezi huu, kuna usiku ulio bora kuliko miezi elfu. Atakayenyimwa kheri zake, basi hakika amenyimwa!)) [An-Nasaaiy]

Comments
Post a Comment